Ujumbe Muhimu Uliolengwa

 

1. Maradhi ya moyo yanazidi kuongezeka. 
Ndio kisababishi kikuu cha vifo miongoni mwa wanawake duniani kote. 

 

Lopez et al. Int J Epidemiol, 2019, 1815-1823.

 

2. Dalili za mshtuko wa moyo hazitambuliki katika zaidi ya 50% ya wanawake.

 

 

DALILI ZA MSHTUKO WA MOYO ZINAZORIPOTIWA MARA NYINGI MIONGONI MWA WANAWAKE

  • Maumivu au usumbufu kwenye kifua 
    (mfano shinikizo, kubanwa, au mchomo) 
  • Maumivu kwenye taya, shingo, mkono, au mgongo
  • Kutokwa na jasho kupita kiasi
  • Kupumua kwa shida
  • Maumivu au usumbufu tumboni, au hisia za kichefuchefu au tatizo la umeng’enyaji wa chakula

 

DALILI ZINGINE ZINAZOAMBATANA AU ZINAZOHUSIANA NA MSHTUKO WA MOYO 

  • Udhaifu au uchovu usio wa kawaida
  • Maumivu ya mgongo, bega au mkono wa kulia
  • Kukosa usingizi
  • Kizunguzungu au kisunzi
  • Mpigo wa moyo ulio wa kasi au usio wa kawaida

 

Lichtman JH, et al. Circulation. 2018;137:781–790.

 

3. Aina ya maradhi ya moyo yanaweza kuwa tofauti kati ya wanawake na wanaume.

 

Aina ya maradhi ya moyo yanayopatikana zaidi: 

  • Maradhi ya ateri za moyo
  • Maradhi ya valvu za moyo
  • Arrhythmia (mpigo wa moyo usio wa kawaida)

Kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa wanawake kuliko wanaume kuwa na hali zifuatazo: 

  • Kupasuka kwa ateri ya moyo (SCAD)
  • Ateri za moyo kuwa nyembamba
  • Kutofanya kazi kwa mishipa midogo (ugonjwa wa mishipa midogo)
  • Cardiomyopathy (ugonjwa wa misuli ya moyo) ya aina ya takotsubo (inayosababishwa na mfadhaiko)
  • Peripartum cardiomyopathy (moyo kudhoofika wakati wa au baada ya ujauzito)
 

 

Norris CM, et al. J Am Heart Assoc 2020 Feb 16; 9(4): e015634.

 

4. Wanawake wanaweza kuwa katika hatari kubwa zaidi ya maradhi ya moyo kuliko wanaume.

 

Hali zifuatazo husababisha hatari kubwa zaidi ya maradhi ya moyo:

 

Matatizo fulani ya ujauzito 
(mf. Kujifungua kabla ya muda, kisukari au shinikizo la damu wakati wa ujauzito, preeclampsia)

Kukoma hedhi mapema
(Wastani wa umri wa kukoma hedhi ni 50-52)

 

Ugonjwa wa uvimbe wa ovari

Magonjwa ya kimfumo ya uvimbe
na kinga nafsia 

(mfano. Rheumatoid arthritis, lupus)

Uvutaji sigara
(Wanawake wana hatari mara 3 zaidi ya wanaume kupata mshtuko wa moyo kutokana na uvutaji sigara)

Ugonjwa wa kisukari
(Kuna uwezekano mara 3 zaidi wanawake wanaoishi na kisukari kufa kutokana na ugonjwa wa moyo ikilinganishawa na wanaume)

Garcia, M. et al. (2016). Circ Res, 118(8), 1273-1293.
Yusuf, S. et al. (2004). Lancet, 364(9438): 937-52.

 

5. Kuna mengi ambayo sote tunaweza kufanya ili kusaidia kupunguza hatari.
Maradhi ya moyo yanaweza kuzuilika kwa kiasi kikubwa.

 

Fanya mazoezi ili kudumisha afya bora

Kula vyakula mbalimbali vyenye afya

Dhibiti mfadhaiko

Ishi bila tumbaku ya dukani na uvutaji wa mvuke

Punguza pombe

Pima afya mara kwa mara
(Pimwa kiwango cha sukari kwenye damu, shinikizo la damu na kolesteroli)

Hu, F. B., et al (2000). New England Journal of Medicine, 343(8), 530-537. 
Yusuf, S. et al. (2004). Lancet, 364(9438): 937-52.

 

Ili uwatunze wengine, ni lazima kwanza ujitunze wewe mwenyewe.